Karibu
Kwa niaba ya Bodi ya Wakurugenzi, Menejimenti na Watumishi wa Kampuni ya Mbolea Tanzania TFC, Nawakaribisha katika tovuti yetu ili ufahamu masuala mbalimbali juu ya mbolea bora na huduma zinazotolewa na Kampuni.
Kampuni ya Mbolea Tanzania (Tanzania Fertilizer Company – TFC) ilianzishwa tarehe 6 Julai, 1968 chini ya Sheria ya Makampuni (Companies Ordinance CAP 212) ambayo kwa sasa inafahamika kama Sheria ya Makampuni ya mwaka 2002 (Companies Act 2002 CAP 212);
Kama Dira yetu inavyoeleza kuwa Kmpuni inayoongoza katika usambazaji wa mbolea, Malengo yetu ni kuwa kampuni bora ya Serikali inayozalisha, kusambaza na kuuza mbolea bora kwa bei nafuu ili kuwapa unafuu wakulima. Kutoa taarifa za kitaalam zinazohusiana na uzalishaji, ubora na viwango vya mbolea ndani na nje ya Nchi. Na kwa kushirikiana na Taasisi za utafiti kufanya utafiti juu ya masuala ya mbolea na pembejeo nyingine za kilimo hapa Nchini.
Asante kwa kutembelea tovuti yetu.
Bw. Samuel A. Mshote
MKURUGENZI MKUU