Kampuni ya Mbolea Tanzania (Tanzania Fertilizer Company – TFC)
ilianzishwa tarehe 6 Julai, 1968 chini ya Sheria ya Makampuni (Companies Ordinance CAP 212) ambayo
kwa sasa inafahamika kama Sheria ya Makampuni ya mwaka 2002 (Companies Act 2002 CAP 212);
Mwaka 1972, Serikali ilizindua kiwanda Mkoani Tanga cha kuzalisha tani 105,000 za mbolea kwa mwaka
aina za Tri-Super Phosphate (TSP), Single Super Phosphate (SSP) na mbolea za mchanganyiko za
NPK ambacho kiliendeshwa na Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC)
Mwaka 1980, usimamizi wa Kampuni ulihamishiwa Shirika la Maendeleo ya
Viwanda Vya Kemikali (National Chemical Industries –NCI).
Kufuatia hitilafu ya mitambo, Aprili 1991, shughuli za uzalishaji wa mbolea zilisitishwa na Serikali
iliamua kufunga Kiwanda hicho na wafanyakazi waliachishwa kazi kupitia Waraka Na. 6 wa Baraza la
Mawaziri wa mwaka 1996

