Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Kilimo

Kampuni ya Mbolea Tanzania

TFC YASHIRIKI KATIKA MAONESHO YA 49 YA BIASHARA YA KIMATAIFA

Imewekwa: 08 Jul, 2025
TFC YASHIRIKI KATIKA MAONESHO YA 49 YA BIASHARA YA KIMATAIFA

Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) tunaendelea kuwakaribisha wakulima, wafanyabiashara na wadau wote wa sekta ya Kilimo katika banda letu, lililopo ndani ya banda la Wizara ya Kilimo kwenye Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayoendelea katika Viwanja vya Mwl. J. K Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.

Karibu ujifunze juu ya Elimu ya Mbolea, aina za mbolea, matumizi sahihi ya mbolea kulingana na aina ya udongo na faida za kutumia mbolea ili kuwa na uzalishaji wenye tija.

Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa (Sabsaba) yalianza rasmi tarehe 28 Juni 2025 na yanatarajiwa kuhitimishwa tarehe 13 Julai 2025.