Accessibility Settings

Text Size

Color Contrast

Language

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Kilimo

Kampuni ya Mbolea Tanzania

/ Kuuza Mbolea

Kuuza Mbolea

Katika kufikia malengo ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwafikia wakulima kwa pembejeo za ruzuku, Wizara ya Kilimo kupitia Kampuni ya Mbolea Tanzania imefanikiwa kusambaza mbolea ya ruzuku na kuwafikia wakulima zaidi ya 950,000 kutoka wakulima 57,000 wakati Mhe. Rais akiingia madarakani.

Aidha katika kipindi cha Uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan ameiwezesha TFC kuipatia mtaji uliosaidia kurejesha shughuli za Kampuni ikiwa ni kuuza na kusambaza mbolea kwa wakulima wote nchini kwa bei ya ruzuku na kuwafikia wakulima kwenye mikoa yote nchini. TFC kwa mwaka wa fedha 2024/2025 imefanikiwa kuagiza mbolea za mazao ya chakula jumla ya tani 70,500 ambazo ni mbolea ya DAP tani 49,500, UREA tani 11,000 na CAN tani 10,000. Upatikanaji wa mbolea ya ruzuku, umewezesha kwa kiasi kikubwa sana kuongeza kwa uzalishaji wa mazao ya chakula kutoka tani 17,148,290 mwaka 2021/2022 hadi kufikia tani 22,803,316 mwaka 2024/2025 sawa na ongezeko la asilimia 33 na kufanya utoshelevu wa chakula nchini kufikia asilimia 128 dhidi ya lengo la asilimia 13.

Pamoja na hayo TFC imeweza kusambaza mbolea kwenye mazao ya biashara mfano zao la tumbaku, kutokana na mafanikio hayo katika msimu wa kilimo mwaka 2024/2025 wakulima wa zao la tumbaku nchini, wamewezeshwa mbolea ya ruzuku zaidi ya tani 59,127 hali iliyopelekea kuondoa changamoto za ucheleweshaji wa mbolea kwa wakulima wa zao hilo na kuongeza mavuno. Maamuzi ya Serikali, kupitia Wizara ya Kilimo ya kuitaka TFC isambaze mbolea ya zao la tumbaku ni hatua bora kwa Taifa kwenye soko la kigeni ambapo katika msimu wa kilimo wa mwaka 2024/2025 takribani tani 160,000 za tumbaku zimezalishwa sawa na ongezeko la asilimia173.47.

 

‘TFC Mbolea Bora’