Accessibility Settings

Text Size

Color Contrast

Language

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Kilimo

Kampuni ya Mbolea Tanzania

/ News

Minister for Agriculture Meets Maniema Governor to Strengthen Agricultural Cooperation

Imewekwa: 03 March, 2026
Minister for Agriculture Meets Maniema Governor to Strengthen Agricultural Cooperation

Waziri wa Kilimo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Daniel Chongolo, amefanya kikao na Gavana wa Jimbo la Maniema, Moise Mussa Kabwankubi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), kwa lengo la kujadili maeneo ya ushirikiano katika sekta ya kilimo kati ya Tanzania na DRC.

Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa ofisi za Tanzania Fertilizer Company (TFC) na kuhudhuriwa na ugeni kutoka Ubalozi wa Congo, wawakilishi wa Serikali ya Tanzania pamoja na wafanyakazi wa TFC. Katika mazungumzo yao, viongozi hao wamejadili uwezekano wa kupanua ushirikiano wa kilimo ili kuongeza uingizaji wa bidhaa za kilimo kutoka Tanzania kwenda Jimbo la Maniema nchini DRC. Ushirikiano huo unatarajiwa kufungua masoko mapya kwa wakulima na wazalishaji wa Tanzania pamoja na kuimarisha biashara ya mipakani kati ya nchi hizo mbili.

TFC imeendelea kuwa mdau muhimu katika kuchochea maendeleo ya sekta ya kilimo kupitia usambazaji wa pembejeo na kushiriki katika majadiliano ya kimkakati yanayolenga kukuza uzalishaji na masoko ya mazao ndani na nje ya nchi. Hatua hii inaakisi dhamira ya Serikali ya Tanzania na DRC katika kuimarisha mahusiano ya kiuchumi na kukuza sekta ya kilimo kama nguzo muhimu ya maendeleo endelevu ya kikanda.