Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Kilimo

Kampuni ya Mbolea Tanzania

Mkurugenzi wa Biashara (TFC) akipokea POS kutoka kwa Waziri wa Kilimo.

Imewekwa: 09 May, 2024
Mkurugenzi wa Biashara (TFC) akipokea POS kutoka kwa Waziri wa Kilimo.

Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein M. Bashe (Mb) akimkabidhi Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Biashara wa Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) Ndg. Lameck Borega kishikwambi vilivyotolewa na Wizara ya Kilimo kwa lengo la kurahisisha usajili wa wakulima katika mifumo ya ugawaji wa pembejeo na upimaji wa afya ya udongo.

Akikabidhi vishikwambi 3500 na POS kwa Maafisa Ugani Kilimo, Mhe. Hussein Bashe ameeleza kuwa Wizara ya Kilimo imeazimia kuhakikisha kuwa miradi ya kilimo inatekelezwa ipasavyo ili kuweza kumnufaisha mkulima na kufikia lengo la Serikali la kuchangia Pato la Taifa kwa asilimia 10 huku ikilenga kufikia bilioni 2.3 ya mauzo ya mazao nchi za nje.

Hafla hiyo ya Uzinduzi wa Ugawaji wa Vishikwambi na POS Kwa Maafisa Ugani Kilimo na Mawakala wa Pembejeo za Kilimo Mtumba, imefanyika jijini Dodoma leo tarehe 7 Mei, 2024 na kuhudhuriwa na Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Makatibu Tawala.