Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mbolea Tanzania, Bw. Samuel Mshote, akisimamia ufungashaji wa Mbolea tayari kupelekwa kwa wakulima.
Imewekwa: 28 January, 2026
Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) imeendelea kutekeleza mkakati wa Serikali wa kuhakikisha upatikanaji wa mbolea kwa wakati kwa wakulima nchini, kufuatia uingizaji wa tani 50,000 za mbolea aina ya DAP kwa ajili ya msimu wa kilimo unaoendelea. Hatua hii inalenga kuongeza tija katika uzalishaji wa mazao na kuimarisha usalama wa chakula nchini.

