Accessibility Settings

Text Size

Color Contrast

Language

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Kilimo

Kampuni ya Mbolea Tanzania

/ News

TFC YAPATA HATI SAFI MWAKA WA FEDHA 2024/2025

Imewekwa: 18 July, 2026
TFC YAPATA HATI SAFI MWAKA WA FEDHA 2024/2025

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) Bw. Samuel Mshote amewataka watumishi kujituma, kufanya kazi kwa bidii, kujitathmini katika utendaji kazi na kila mmoja kuwa balozi katika nafasi yake ili kufikia malengo ya taasisi.

Amebainisha hayo katika kikao cha watumishi wa makao makuu, kilichofanyika leo Julai 10, 2026, jijini Dar es salaam ambapo amepongeza mafanikio ya Taasisi yaliyopatikana kwa mwaka wa fedha 2025/2026 ikiwemo hati safi ya Mkaguzi wa Nje (CAG) kwa mwaka wa fedha 2024/2025

Ameeleza kuwa utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya mwaka 2050 umeanza na TFC chini ya Wizara ya Kilimo yapo maeneo yanayopaswa kutekezwa ili kuongeza tija katika uzalishaji wa mazao na nchi kuwa na utoshelevu wa chakula.

Aidha, katika utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2026/2027 amewataka watumishi kuzingatia vipaumbele sita (06) vya Wizara ambapo TFC ipo katika kutekeleza kipaumbele namba moja cha kuongeza tija na uzalishaji kwa kusambaza mbolea tani 150,000 za mazao ya chakula, tani 70,000 za mbolea ya tumbaku tani 500 za zao la chai na tani 50,000 za wazalishaji wa ndani ya nchi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma za Taasisi Bi. Nuru Mhando amesisitiza juu ya kufuta hoja za ukaguzi ili kuendelea kupata Hati Safi na kuzingatia ujazaji wa PEPMIS ili kila mtumishi aweze kupimwa katika utendaji kazi 

Mkurugenzi wa Uendeshaji Biashara Bw. Lameck Borega ameeleza kuwa sifa ya Kampuni ya Biashara ni kupunguza matumizi, kubuni vyanzo vipya vya mapato na kuongeza kasi ya kutafuta masoko.

slot gacor