TFC Yashiriki Kikao cha Wadau wa Kilimo Wilaya ya Mbogwe, Geita
Imewekwa: 03 February, 2026
Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) imeshiriki kikao cha wadau wa kilimo kilichofanyika Wilaya ya Mbogwe, Mkoa wa Geita, kikiongozwa na Mkuu wa Wilaya, Mheshimiwa Sakina Mohammed. Kikao hicho kililenga kujenga uelewa wa pamoja kuhusu changamoto za wakulima na kuimarisha ushirikiano kati ya taasisi zinazohudumia sekta ya kilimo. TFC iliwahakikishia wakulima upatikanaji wa mbolea kwa wakati ili kuendana na mahitaji ya msimu wa kilimo.

