TFC YASHIRIKI MAONESHO YA AFRICA AGRI EXPO 2026, YATOA ELIMU YA MBOLEA KWA WADAU NA WAWEKEZAJI
Imewekwa: 09 September, 2026
Kampuni ya Mbolea Tanzania(TFC), imeshiriki Maonesho ya 10 ya Kilimo Africa 2026 (Africa Agri Expo 2026), ambapo wadau wa kilimo waliotembelea wamepata fursa ya kujifunza juu ya elimu ya matumizi sahihi ya mbolea.
Maonesho haya yamewakutanisha zaidi ya kampuni 120 kutoka nchi zaidi ya 35 ambapo wadau na wananchi mbalimbali wameelimishwa juu ya umuhimu wa kutumia mbolea, matumizi sahihi ya mbolea na aina za mbolea zinazoagizwa na kusambazwa na TFC.
Maonesho yamefanyika katika Viwanja vya Maonesho vya Mwalimu Julius Nyerere (Tantrade ), Jijini Dar es Salaam, yalianza tarehe 2 Septemba 2026 na kuhitimishwa leo tarehe Septemba 3, 2026.

