Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Kilimo

Kampuni ya Mbolea Tanzania

MENEJIMENTI YA TFC YATAKIWA KUANGALIA ZAIDI HITAJI LA WADAU

Imewekwa: 14 Jun, 2025
MENEJIMENTI YA TFC YATAKIWA KUANGALIA ZAIDI HITAJI LA WADAU

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) Bw. Samuel Mshote ameeleza kuwa kuelekea mwaka mpya wa fedha na msimu ujao wa kilimo 2025/2026 TFC inatakiwa kuhakikisha inatekeleza jukumu la usambazaji wa mbolea kwa wakulima, kwa wakati sambamba na kuhakikisha inaondoa hoja za ukaguzi.

Akizungumza katika kikao cha Menejimenti, kilichokutana kwaajili ya kupitia hoja za ukaguzi kwakipindi cha robo ya tatu, Januari-Machi, 2024/2025, kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi, Bw. Mshote ameeleza kuwa Serikali kupitia Wizara ya Kilimo imeiamini TFC kuwadumia wakulima kwennye sekta ya mbolea na pembejeo zingine hivyo kuelekea msimu ujao wa kilimo kila ni jukumu la kila mtumishi kufanya kazi kwa bidii na kuhakikisha malengo hayo yanafikiwa.

Wakieleza juu ya tathmini ya ukaguzi waliofanya, Wakaguzi wa Ndani wa Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) wameeleza kuwa ni vema TFC ikajikita katika utoaji wa elimu kwa wakulima ili wakulima wafahamu zaidi juu ya aina za mbolea, afya za udongo na matumizi sahihi ya mbolea. Aidha katika kutoa huduma ya aina za mbolea, ni vema TFC ikaangalia uhitaji wa wakulima kwakuwa ndio watumiaji wa mbolea hizo.