Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Kilimo

Kampuni ya Mbolea Tanzania

WATUMISHI TFC WAHIMIZWA KUFANYA KAZI KWA BIDII ILI KUFIKIA MALENGO YA TAASISI

Imewekwa: 19 May, 2025
WATUMISHI TFC WAHIMIZWA KUFANYA KAZI KWA BIDII ILI KUFIKIA MALENGO YA TAASISI

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) Bw. Samuel Mshote amewasihi watumishi wa TFC kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa ufanisi ili kufikia malengo.

Akizungumza katika kikao cha Menejimenti, kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano, Bw. Mshote ameeleza kuwa Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) inalo jukumu kubwa la kuhakikisha mbolea za ruzuku inawafikia wakulima kwa wakati ili kutekeleza ahadi ya Serikali kwa wakulima.

Ameongeza kuwa kama ambavyo TFC imeaminiwa na Serikali katika kuuza na kusambaza mbolea ya ruzuku kwa wakulima ni wajibu wa kila mtumishi katika nafasi yake kuhakikisha anatekeleza majukumu ili kuleta matokeo tarajiwa.

Katika kikao hicho, iliwasilishwa taarifa ya usambazaji wa mbolea ya ruzuku sambamba na taarifa za miradi mbalimbali inayotarajiwa na inayoendelea kutekelezwa ukiwemo mradi wa kiwanda cha kuchanganya mbolea (blending facilities) unaotarajia kukamilika mwishoni mwa mwaka huu.