Accessibility Settings

Text Size

Color Contrast

Language

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Kilimo

Kampuni ya Mbolea Tanzania

/ News

TFC yelekezwa kuimarisha upatikanaji wa Mbolea kwa Wakulima

Imewekwa: 04 May, 2026
TFC yelekezwa kuimarisha upatikanaji wa Mbolea kwa Wakulima

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo anayesimamia Maendeleo ya Mazao na Usalama wa Chakula, Prof. Peter L. Msoffe, ameielekeza TFC kuimarisha upatikanaji wa mbolea ili kuhakikisha uzalishaji wa kilimo haukatizwi, akisisitiza kuwa usalama wa chakula ni kipaumbele cha taifa.

Pia ameitaka TFC kushirikiana na Halmashauri kuzalisha mbolea za asili kutokana na taka na kuvutia wawekezaji kuongeza uzalishaji wa ndani. Mkurugenzi Mkuu wa TFC, Bw. Samuel Mshote, ameahidi upatikanaji wa mbolea kwa wakati licha ya changamoto za nje.