TFC YAENDELEA NA ELIMU YA MATUMIZI SAHIHI YA MBOLEA KWA VITENDO
Kampuni ya Tanzania (TFC) inaendelea kutekeleza mpango wa kutoa elimu kwa wakulima na uhamasishaji wa matumizi sahihi ya mbolea kwa vitendo kupitia shamba darasa.
Hili ni shamba la mahindi la Mkulima Godfrey Massawe, lenye ukubwa wa hekari 4, ambalo pia ni moja ya shamba darasa la TFC lililopo Mkoani Kilimanjaro, Wilaya ya Hai, Kata ya Weruweru, eneo la Mailisita.
Mkulima huyu baada ya kufundishwa elimu ya matumizi sahihi ya mbolea kwa nadharia, ameamua pia kutumia mbolea za TFC kwa kufuata kanuni nne za mbolea matumizi sahihi ya mbolea.
TFC inaendelea kusimamia kwa umakini hatua zote uwekaji wa mbolea kwenye shamba hilo kuanzia mbolea ya kupandia mazao aina ya DAP 46%P, mbolea ya kukuzia mazao aina ya Urea 46%N na mbolea ya kubebeshea mazao CAN%27N.
Mkulima huyu pamoja na wakulima jirani walipokea elimu hiyo na kuitekeleza kwa vitendo na leo Wataalam wa TFC wamefika shambani hapo na kushiriki katika zoezi la kuweka mbolea ya kukuzia ya UREA 46%N.

