Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Kilimo

Kampuni ya Mbolea Tanzania

KAMPUNI ZA MBOLEA ZA TANZANIA NA ZAMBIA ZASAINI MKATABA WA BIASHARA

Imewekwa: 12 Jun, 2025
KAMPUNI ZA MBOLEA ZA TANZANIA NA ZAMBIA ZASAINI MKATABA WA BIASHARA

Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) imesaini mikataba na Kampuni ya United Capital Fertilizer Limited kwaajili ya mauziano ya mbolea aina ya NPK 10:18:24, UREA na CAN.Hafla hiyo imefanyika tarehe 11Juni 2025, katika Ukumbi wa Wizara ya Kilimo, Jijini Dodoma.

Utiaji saini wa makubaliano hayo ya kibiashara ni kati ya Bw. Samuel Mshote, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) na Bw. Huang Yaachi, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya United Capital Fertilizer Limited (UCFL) ya nchini Zambia ambapo hii ni ishara ya mwendelezo wa biashara ya uuzaji wa mbolea ya ruzuku baina ya Kampuni hizo mbili