Accessibility Settings

Text Size

Color Contrast

Language

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Kilimo

Kampuni ya Mbolea Tanzania

/ News

TANZANIA NA MISRI KUENDELEZA USHIRIKIANO KATIKA SEKTA KILIMO,BIASHARA, AFYA,MAJI NA UWEKEZAJI

Imewekwa: 20 July, 2026
TANZANIA NA MISRI KUENDELEZA USHIRIKIANO KATIKA SEKTA KILIMO,BIASHARA, AFYA,MAJI NA UWEKEZAJI

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) Bw. Samuel Mshote ni miongoni mwa washiriki wa jukwaa la Biashara la Tanzania na Misri, lililowakutanisha wafanyabiashara na wawekezaji kutoka nchi mbili, kwa lengo la kujadili fursa za biashara na uwekezaji.

Jukwaa hili linalofanyika tarehe leo Julai 18, 2026 katika Hoteli ya Hyatt Regency, Dar es Salaam ni sehemu ya ziara ya kiserikali ya Rais wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, Mhe. Abdel Fattah El-Sisi nchini Tanzania kwa lengo la kuwakutanisha viongozi wa Serikali, wawekezaji, wafanyabiashara wa nchi za Tanzania na Misri ili kujadili na kuimarisha ushirikiano katika sekta mbalimbali ikiwemo kilimo, biashara, uwekezaji, afya, maji, elimu na miundombinu.

Tanzania na Misri zinaendelea kushirikiana katika sekta mbalimbali, hususan utekelezaji wa miradi ya maendeleo, mafunzo ya wataalamu na kubadilishana uzoefu. Hivyo kupitia jukwaa hili Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) inatarajia kuimairisha uhusiano wa biashara ya mbolea na wawekezaji wa sekta ya mbolea wa nchini Misri.

slot gacor