Kikao cha Ngazi ya Juu cha Kuimarisha Biashara ya Kilimo kati ya Tanzania na DRC Chafanyika Ofisi za TFC
Imewekwa: 03 March, 2026
Waziri wa Kilimo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Daniel Chongolo, amefanya mazungumzo na Gavana wa Jimbo la Maniema kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Moise Mussa Kabwankubi, kwa lengo la kuimarisha ushirikiano wa kilimo kati ya Tanzania na DRC.
Kikao hicho kilifanyika katika ofisi za Tanzania Fertilizer Company (TFC) na kuhudhuriwa na ujumbe kutoka Ubalozi wa Congo, Serikali ya Tanzania pamoja na wafanyakazi wa TFC.
Pande zote zimejadili kuongeza biashara ya mazao ya kilimo kutoka Tanzania kwenda Maniema, hatua inayolenga kupanua masoko, kuongeza thamani ya mazao ya wakulima na kukuza uchumi wa kikanda.

