Accessibility Settings

Text Size

Color Contrast

Language

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Kilimo

Kampuni ya Mbolea Tanzania

/ News

MBOLEA ZA RUZUKU ZATOA AJIRA KWA VIJANA

Imewekwa: 23 November, 2026
MBOLEA ZA RUZUKU ZATOA AJIRA KWA VIJANA

Upatikanaji na usambazaji wa mbolea za ruzuku kupitia Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) katika Mkoa wa Rukwa umefungua fursa za ajira kwa vijana, kuongeza kipato kwa wafanyabiashara na kuchochea shughulı za kiuchumi katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo.
Afisa Masoko wa TFC Mkoa wa Rukwa, Shira Mkisi, amesema uwepo wa mbolea hizo umewawezesha vijana kupata ajira katika shughuli za kupakia na kushusha mizigo, huku wafanyabiashara wadogo, wakiwemo wauza chakula, wakinufaika na ongezeko la wateja wanaotokana na shughuli hizo.
Amesema hatua hiyo ni sehemu ya juhudi za Serikali chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, kupitia Wizara ya Kilimo, kuhakikisha mbolea za ruzuku zinapatikana kwa wakulima na kuchochea maendeleo ya sekta ya kilimo.
Kwa upande wao, baadhi ya vijana wanaofanya kazi za kupakia na kushusha mbolea wameishukuru Serikali kwa kuwapatia fursa hiyo ya kujipatia kipato, kwani kazi hiyo imewawezesha kutunza familia na kusomesha watoto

slot gacor