Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Kilimo

Kampuni ya Mbolea Tanzania

MBOLEA YA RUZUKU YAWAFIKIA WAKULIMA NCHINI

Imewekwa: 21 May, 2025
MBOLEA YA RUZUKU YAWAFIKIA WAKULIMA NCHINI

Kuelekea uwasilishaji wa Bajeti ya Wizara ya Kilimo, kwa mwaka wa fedha 2025/2026, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) Bw. Samuel Mshote (wa kwanza kutoka kulia) ameeleza juu ya utekelezaji wa bajeti inayoendelea na mikakati ya bajeti ya mwaka 2025/2026 katika kipindi cha Clouds 360 kinachorushwa na Clouds TV.

Katika maelezo yake Bw. Mshote ameeleza kuwa zaidi ya tani 78,000 za mbolea ya ruzuku zimeingizwa nchini na kusambazwa kwa wakulima ambao ndio wanufaika na mbolea hiyo ya ruzuku.

Bajeti ya Wizara ya Kilimo ya mwaka wa fedha 2025/2026 inatarajiwa kuwasilishwa leo tarehe 21-22.05.2025 na Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe (Mb).