Rukwa: Wakulima Wahamasishwa Kuongeza Matumizi ya Mbolea kwa Uzalishaji Bora
Imewekwa: 03 March, 2026
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mhe. Charles Makongoro Nyerere, amepongeza jitihada za wakulima kutumia Mbolea na kuhimiza Ushirikiano na Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) kuhakikisha pembejeo zinawafikia kwa wakati.
Katika kikao cha kitaalamu kilichohudhuriwa na Mkurugenzi Mkuu, Ndg. Samuel Mshote, Mkurugenzi wa Uendeshaji Biashara, Ndg. Lameck Borega, na Mtaalam wa Kilimo, Ndg. Daud Siarra, amesisitiza kuwa matumizi sahihi ya Mbolea ni muhimu kuongeza tija, kukidhi mahitaji ya mahindi, na kuwezesha mauzo ya ziada nje ya Nchi. Kwa msimu wa 2025/2026, jumla ya tani 9,470 za mbolea kutoka TFC zimesambazwa Mkoa wa Rukwa.

