KIKAO CHA KAMATI YA MIPANGO, UWEKEZAJI NA UTAWALA KUJADILI MPANGO NA BAJETI YA TFC MWAKA WA FEDHA 2025/2026
Katika kikao maalumu, kujadili Mpango na Bajeti ya Kampuni ya Mbolea Tanzania kwa mwaka wa fedha 2026/2027 wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi Kamati ya Mipango, Uwekezaji na Utawala, wameitaka Menejiment kuwa na mipango endelevu ya utekelezaji wa majukumu yake ili kufikia malengo yanayopangwa katika Mpango na Bajeti ya Taasisi.
Wakizungumza katika kikao hicho kilichofanyika leo Machi 27, 2026 katika ukumbi wa ofisi za TFC, jijini Dar es salaam, wajumbe hao wamesisitiza juu ya Mpango na Bajeti kuwa na malengo yanayopimika na utekelezaji wa majukumu ubainishe hatua iliyofikiwa.
Aidha, wajumbe wameshauri kuwa TFC iimarishe ushirikiano na wadau wa kilimo, mfano wadau wa zao la pamba ili kupata ufahamu juu ya mbolea wanazotumia katika uzalishaji wa zao hilo ili kuipa nafasi Kampuni kusambaza mbolea kwa wadau hao.
Mwisho, wajumbe wameidhinisha makadirio ya Mpango na Bajeti ya mwaka 2026/2027 huku wakisitiza juu ya utekelezaji wa Sera ya Kampuni, kujikita katika jukumu la msingi ambalo ni kuuza na kusambaza mbolea kwa wakulima ili wanufaike na kuzalisha kwa tija kama Serikali ilivyokusudia kuwa na utoshelevu wa chakula.

