Accessibility Settings

Text Size

Color Contrast

Language

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Kilimo

Kampuni ya Mbolea Tanzania

/ News

The Fertilizer is ready to be distributed to farmers across the country.

Imewekwa: 29 January, 2026
The Fertilizer is ready to be distributed to farmers across the country.

Hatua hii inalenga kuhakikisha upatikanaji wa pembejeo muhimu za kilimo kwa wakati, hususan kabla ya kuanza kwa msimu wa kilimo, ili kuongeza tija, uzalishaji, na usalama wa chakula nchini.

Mpango wa usambazaji umeandaliwa kwa kuzingatia uwiano wa mahitaji ya mikoa yote nchini, kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo wasambazaji, na taasisi husika. Taratibu na mifumo madhubuti imewekwa ili kuhakikisha usambazaji unafanyika kwa uwazi, ufanisi, na kwa kuzingatia kanuni na miongozo iliyopo. Wakulima wanahimizwa kufuata maelekezo yatakayotolewa na Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC), na mamlaka za serikali kuhusu upatikanaji na matumizi sahihi ya mbolea. Usimamizi wa utekelezaji wa mpango huu utaendelea kufanyika ili kuhakikisha malengo ya kuimarisha sekta ya kilimo, kuongeza kipato cha wakulima, na kukuza uchumi wa taifa yanafikiwa.