KAMPUNI YA MAADEN YA NCHINI SAUDI ARABIA KUSHIRIKIANA NA TFC KATIKA USAMBAZAJI WA MBOLEA KWA WAKULIMA
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) Bw. Samuel Mshote amefanya mazungumzo na uongozi wa Kampuni ya Maaden ya Nchini Saudi Arabia kujadili namna bora ya kuimarisha mahusiano ya biashara ya mbolea.
Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika leo Julai 09, 2016 Bw. Mshote ameeleza kuwa katika kutekeleza dira ya Agenda 10/30 TFC inajukumu la kuhakikisha upatikanaji na usambazaji wa mbolea kwa wakulima wote nchini. Hivyo kuelekea msimu mpya wa kilimo 2026/2027, TFC imejipanga kufikisha mbolea kwa wakulima kabla ya msimu wa kilimo kuanza.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Maaden kanda ya Afrika, Bw. Roscoe Gehle ameeleza kuwa wapo tayari kushirikiana na TFC katika kuimarisha biashara ya mbolea ndani na nje ya nchi ya Tanzania.
Mazungumzo hayo yamefanyika katika ofisi za TFC, jijini Dar es salaam na kuhusisha ushiriki wa wataalamu kutoka Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) na Kampuni ya Maaden ya Nchini Saudi Arabia

