Accessibility Settings

Text Size

Color Contrast

Language

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Kilimo

Kampuni ya Mbolea Tanzania

/ News

KAMPUNI YA MBOLEA TANZANIA KATIKA MAONESHO YA KIMATAIFA YA NANENANE

Imewekwa: 03 August, 2026
KAMPUNI YA MBOLEA TANZANIA KATIKA MAONESHO YA KIMATAIFA YA NANENANE

Katika hotuba ya ufunguzi wa Maonesho ya Kimataifa ya Nanenane, Waziri Mkuu, Dk. Mwigulu Nchemba, amesema serikali imeendelea kuimarisha sekta ya kilimo kupitia utoaji wa ruzuku ya pembejeo za kilimo, ambapo tangu Rais Dk. Samia Suluhu Hassan aingie madarakani, wakulima wamepatiwa tani 762,175.115 za mbolea, zenye thamani ya zaidi ya shilingi trilioni 1.4.
Akizungumza leo, Agosti 1, 2026, jijini Dodoma, katika ufunguzi wa Maonesho ya Sıkukuu ya Wakulima (Nanenane), Dk. Mwigulu amesema, ruzuku hiyo si mkopo, bali ni fedha zinazotolewa na serikali ili kuwawezesha wakulima kuongeza uzalishaji na tija katika shughuli zao za kilimo.
Aidha, amesema uwekezaji huo umeleta matokeo chanya, ikiwemo kuongezeka kwa uzalishaji wa chakula hadi kufikia utoshelevu wa zaidi ya asilimia 130, hatua inayochangia kuimarisha usalama wa chakula nchini.
Hatua hiyo pia imeongeza mauzo ya mazao nje ya nchi kwa zaidi ya asilimia 77 na kuimarisha akiba ya fedha za kigeni, ambayo kwa sasa inatosheleza zaidi ya miezi minne ya uagizaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi

slot gacor