Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Kilimo

Kampuni ya Mbolea Tanzania

WAKULIMA WA MAHINDI MKOANI RUVUMA WARIDHISHWA NA UBORA WA MBOLEA YA TFC

Imewekwa: 21 May, 2025
WAKULIMA WA MAHINDI MKOANI RUVUMA WARIDHISHWA NA UBORA WA MBOLEA YA TFC

Wakulima wa zao la mahindi wanaojishughulisha na kilimo cha Umwagiliaji, Wilayani Tunduru, Mkoani Ruvuma wameishukuru Serikali ya Awamu ya sita kwa mbolea ya ruzuku inayowawezesha kuendesha kilimo cha kisasa chenye matokeo bora tangu mazao yanapokuwa shambani.

Mmoja wa wakulima hao, Bw. Ali Said Mohamed kutoka kata ya Masonya ameshuhudia namna mbolea ya kupandia ya DAP kutoka Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) ilivyompa matokeo bora, mazao yake yana afya yakuridhisha na matarajio yake ni kuvuna mazao yenye ubora yanayokubalika sokoni.

Pamoja na kuishukuru Serikali, ameiomba TFC kuendelea kuwajali wakulima kwa kuwapa mbolea yenye viwango ili matarajio yao katika kuzalisha mazao bora yafikiwe.