WAKULIMA MKOANI NJOMBE WAHAMASISHWA KUJIUNGA KATIKA MFUMO WA PEMBEJEO ZA RUZUKU
Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) inatekeleza jukumu la kuagiza na kusambaza mbolea ya ruzuku kwa wakulima wote nchini. Pamoja na jukumu hilo TFC inaendelea kumjali mkulima kwa kuhakikisha anapata matokeo bora katika uzalishaji wa mazao!
Bw. Laison Mwaitambila, mkulima wa mazao ya mbogamboga, anayefanyia shughuli za kilimo eneo la Mtewele, wilaya ya Makambako, Mkoa wa Njombe ameeleza kuwa tangu aanze kufuata kanuni bora za kilimo na kuzingatia ushauri wa kitaalamu ameongeza uzalishaji wa mazao, kwasasa anavuna kuanzia gunia 70 mpaka 100 za vitunguu kwa ekari moja.
Bw. Mwaitambila ametoa rai kwa wakulima wenzake kujisajili katika mfumo wa pembejeo za ruzuku ili wanufaike na mbolea za ruzuku. Pia kufuata kanuni bora za matumizi sahihi ya mbolea na kuzingatia ushauri wa kitaalamu ili kuzalisha kwa tija na kupata matokeo bora.
Kwa upande wake Afisa wa TFC, Wilaya ya Makambako Wipa Sanga ameeleza kuwa pamoja na kusambaza mbolea kwa wakulima bado wana wajibu wa kuendelea kuwafuatilia wakulima ili kuona kama wametumia mbolea kwa wakati sahihi na kwa vipimo sahihi.

