Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Kilimo

Kampuni ya Mbolea Tanzania

WAKULIMA MKOANI MBEYA WARIDHISHWA NA UBORA WA MBOLEA ZA TFC

Imewekwa: 19 May, 2025
WAKULIMA MKOANI MBEYA WARIDHISHWA NA UBORA WA MBOLEA ZA TFC

Mazao yanayotumia mbolea za kupandia na kukuzia kutoka Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) yamekuwa ni mazao yenye afya, ukuaji wa kasi na wingi wa mavuno.

Wakulima Mkoani Mbeya wanashuhudia kwa vitendo namna mbolea za TFC zinavyowezesha kilimo chenye tija ili kupata mavuno mengi.

Maafisa kutoka Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) kanda ya Kusini, wamefanya ziara ya kutembelea mashamba ya wakulima katika maeneo ya Uyole, Iyunga na Mbalizi, Manispaa ya Mbeya ili kuona maendeleo ya wakulima hao waliotumia mbolea ya ruzuku ya kupandia ya DAP.

Kwa Mkoa wa Mbeya hadi sasa zaidi ya Tani 4,000 za mbolea ya ruzuku ya kupandia aina ya DAP zimesambazwa kwa wakulima wanaondelea na kilimo cha mahindi, maharage, viazi, mpunga na mbogamboga.