WAKULIMA MKOANI MARA WAISHUKURU SERIKALI KWA MBOLEA YA VIWANGO

Wakulima Mkoani Mara, Wilaya ya Tarime, kutoka kata za Kenyamanyori na Nyandoto wameishukuru Serikali kwa kuwafikishia mbolea ya ruzuku zilizowawezesha kupata matokeo bora.
Mmoja wa wakulima hao, Bw. Mohere Kiiba ameeleza kuwa wakulima wengi waliotumia mbokea za TFC wameridhishwa na viwango vya ubora wa mbolea hizo kutokana na matokeo ya mazao, yana afya na kutarajia kuvuna zaidi ukilinganisha na msimu uliopita.
Afisa Masoko wa Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC), Mkoa wa Mara Bw. Elisha Yaule amewasihi wakulima hao kutoa elimu kwa wakulima wengine ili wafahamu umuhimu wa kutumia mbolea ili kupata matokeo bora.
Hadi sasa mbolea iliyosambaza wilaya ya Tarime na mkoa wa Mara ni zaidi ya tani 1000 na mazao yanayolimwa Wilayani humo ni pamoja na mahindi, maharage, mazao ya mbogamboga na mtama.