USAMBAZAJI WA MBOLEA YA KUPANDIA MAZAO DAP TANI 33,000
Imewekwa: 31 August, 2026
Kuelekea msimu wa kilimo 2026/2027, mbolea ya kupandia mazao aina ya Di Ammonia Phosphate (DAP) inaendelea kusambazwa katika maghala yaliyopo kanda ya Mbeya, Makambako, Sumbawanga, Tabora, Mwanza, Arusha na Songea.
Pia mbolea hiyo imesambazwa katika vituo vya Mauzo vyaTFC vilivyopo Mkoa wa Morogoro, Manyara, Kilimanjaro, Tunduru, Kasulu, Tarime, Kibaigwa, Shinyanga, Geita na Kahama.
Mbolea hii itauzwa kwa bei ya ruzuku hivyo wakulima wote mnakumbushwa kuhuisha taarifa zenu na kujisajiri katika mfumo wa pembejeo za ruzuku.

