Accessibility Settings

Text Size

Color Contrast

Language

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Kilimo

Kampuni ya Mbolea Tanzania

/ News

Naibu Waziri Mallya aipongeza TFC kwa usambazaji wa mbolea ya ruzuku

Imewekwa: 03 August, 2026
Naibu Waziri Mallya aipongeza TFC kwa usambazaji wa mbolea ya ruzuku

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Jemsi Millya, ameipongeza Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) kwa kuendelea kusimamia kwa ufanisi mpango wa mbolea ya ruzuku na kuhakikisha mbolea hiyo inawafikia wakulima kwa wakati.

Mhe. Millya ametoa pongezi hizo leo, Agosti 2, 2026, alipotembelea banda la TFC katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo ya NaneNane yanayoendelea jijini Dodoma.

Akizungumza baada ya kutembelea banda hilo, Mhe. Millya amesema TFC inapaswa kuendelea kusimamia ubora wa mbolea pamoja na usambazaji wake nchini ili kuhakikisha kila mkulima anapata mbolea bora kwa wakati unaofaa.

"Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametenga fedha nyingi kwa ajili ya kuimarisha Kampuni ya Mbolea Tanzania. Hivyo, mnalazimika kufanya kazi kwa weledi, uadilifu na uwajibikaji. 

Aidha, kwa kuwa mna Waziri mwenye maono na mchapakazi, ni muhimu kampuni hii ikaendelea kukua na kutimiza malengo yake ya kuwahudumia wakulima," amesema Mhe. Millya.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TFC, Samuel Mshote, amesema katika mwaka wa fedha 2026/2027 kampuni inatarajia kuagiza tani 270,000 za mbolea za aina mbalimbali. 

Ameongeza kuwa, tani 330,000 tayari zimewasili nchini na zipo bandarini zikiendelea kupakuliwa kabla ya kusambazwa katika vituo vya mauzo nchini.

Mshote amesema kupitia Maonesho ya NaneNane, TFC imejipanga kutoa elimu kuhusu kuhusu matumizi sahihi ya mbolea pamoja na utaratibu wa kupata mbolea ya ruzuku. 

Ametoa wito kwa wananchi na wakulima kutembelea banda la TFC lililopo ndani ya banda kubwa la Wizara ya Kilimo ili kupata elimu na huduma mbalimbali zinazotolewa na kampuni hiyo.

slot gacor