Naibu Waziri wa Kilimo Afanya Kikao Kuhusu Kiwanda cha Mbolea za NPK na UREA
Imewekwa: 03 March, 2026
Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. David Silinde (MB), amefanya kikao na wawekezaji kutoka kampuni ya iGSAS ya nchini Uturuki kuhusu mpango wa kuanzisha kiwanda cha mbolea za NPK na UREA nchini Tanzania. Kushoto akiwa ameketi ni Mkurugenzi wa Uendeshaji Biashara wa Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC), Ndg. Lameck Borega. Kikao kilifanyika tarehe 11 Februari 2026 jijini Dar es Salaam.

