Usambazaji wa Mbolea ya DAP Mkoa wa Rukwa
Imewekwa: 03 February, 2026
Mapokezi na usambazaji wa mbolea ya DAP yanaendelea katika Mkoa wa Rukwa, Manispaa ya Sumbawanga, kwa ajili ya wakulima wanaojiandaa kupanda mazao mbalimbali. Wakulima wanahimizwa kutumia mbolea kwa usahihi ili kuongeza rutuba ya udongo na tija ya uzalishaji.

