KIKAO MAALUM CHA BODI YA WAKURUGENZI
Katika kikao Maalum cha Bodi ya Wakurugenzi, Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) wameitaka Menejiment kuhakikisha mfumo wa kidigitali wa mauzo ya mbolea inatumika ili kuepusha mwanya wa upotevu wa mapato ya Kampuni.
Wito huo umetolewa leo Septemba 07, 2026 katika kikao maalumu kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi za TFC, Jijini Dar es salaam kwa lengo la kujadili Taarifa ya Hali ya Upatikanaji, Ununuzi na Usambazaji wa Mbolea kwa msimu wa kilimo 2026/2027 ambapo wameagiza katika kikao kijacho wapitishwe katika mfumo huo wa mauzo.
Pamoja na hayo, Bodi ya Wakurugenzi imeagiza kufanyika kwa mchanganuo/uchambuzi wa mauzo ya mbolea kwa kila kituo cha mauzo kwa mwaka wa fedha 2025/2026 ili wajumbe hao wafahamu mauzo ya kila kituo. Na kusisitiza kufuata utaratibu wa Mpango wa Manunuzi wakati wa uagizaji wa mbolea.

