Accessibility Settings

Text Size

Color Contrast

Language

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Kilimo

Kampuni ya Mbolea Tanzania

/ News

KIKAO CHA BODI YA WAKURUGENZI KUJADILI MPANGO NA BAJETI YA TFC 2026/2027

Imewekwa: 30 March, 2026
KIKAO CHA BODI YA WAKURUGENZI KUJADILI MPANGO NA BAJETI YA TFC 2026/2027

Katika Kikao maalum cha 4 cha Bodi ya Wakurugenzi kwa mwaka wa fedha 2025/2026 Mwenyekiti wa Bodi Dkt. Florens Turuka na wajumbe wa Bodi wameitaka Menejimenti kutokana na hali ya migogoro inayoendelea duniani kuwa na mikakati itakayowezesha upatikanaji wa mbolea nchini pasipo kutegemea nchi zenye mbolea zinazoathirika na migogoro hiyo.

Akizungumza katika kikao cha kujadili Mpango na Bajeti ya Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) kwa mwaka wa fedha 2026/2027 kilichofanyika  tarehe 28, Machi 2026 katika ukumbi wa ofisi za TFC, jijini Dar es salaam Dkt .Turuka ameeleza kuwa ni vema Kampuni ikajipanga kwa mikakati ya namna ya kuwa na utoshelevu wa mbolea nchini ila kuwapa wakulima uhakika wa pembejeo mbolea.

Katika kikao hicho wajumbe wameendelea kukumbusha juu ya kujikita katika lengo kuu la Kampuni la uuzaji na usambazaji wa mbolea kwa wakulima sambamba na utekelezaji wa miradi ya kipaumbele inayoendana na jukumu la msingi la uagizaji na usambazaji wa mbolea.

Aidha, wameitaka Menejiment kuwa na utaratibu wa kufanya tathmini ya utekelezaji wa bajeti kila mwaka wa fedha unapoisha ili kuona kama malengo yaliyopangwa katika mwaka husika yametekelezwa kama yalivyopangwa.

Mwisho, kwa pamoja wajumbe hao wameridhia na kupitisha Mpango na Bajeti ya Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) kwa mwaka wa fedha 2026/2027.