Tathmini ya Mafanikio ya Matumizi ya Mbolea na Chokaa Mazao kwa wanufaika wa mradi wa TFSRP
Katika ziara ya kutathmini mafanikio utekelezaji wa mradi wa Tanzania Food Systems Resilience Programme (TFSRP) Mikoa ya Njombe na Katavi, Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) imeendelea na zoezi la tathmini kwa kutembelea mashamba ya wakulima wanufaika ili kujionea matokeo ya matumizi ya mbolea mbalimbali ikiwemo chokaa mazao.
Wakulima wanufaika wa mradi huo wameeleza kuridhishwa na matokeo chanya waliyoyapata, na kubainisha kuwa matumizi ya chokaa mazao pamoja na mbolea hizo yameongeza rutuba ya udongo na kuleta matumaini mapya ya mavuno bora.
Aidha, kwa nyakati tofauti tofauti wakulima hao wameishukuru Serikali kwa kuwawezesha kupata pembejeo hizo, na kueleza kuwa hatua hiyo imekuwa chachu ya kuongeza tija katika sekta ya kilimo na kuboresha hali za maisha.

