RUZUKU YA PEMBEJEO ZA KILIMO YAINUA UCHUMI WA FAMILIA IRINGA
Imewekwa: 19 November, 2026
Wakulima Mkoani Iringa, wamesisitizwa kuhakikisha wanajisajili katika Mfumo wa Pembejeo za Ruzuku ili kunufaika na mbolea za ruzuku ambazo tayari zimeanza kusambazwa kwa wakulima wote nchini.
Bw. Yusufu Kangabya, Msimamizi wa Kituo cha Mauzo cha Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) Mkoa wa Iringa amesema kuwa TFC kwa kushirikiana na mawakala imeanza kusambaza mbolea za kupandia mazao aina ya DAP zinazouzwa kwa wakulima kwa bei ya ruzuku.
Kwa upande wake mkulima ambaye pia ni wakala wa pembejeo za kilimo Bi. Irene Kiwango ameeleza kuwa kutokana na kutumia mbolea ameongeza uzalishaji wa mazao na kukuza uchumi wa familia.

