Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Kilimo

Kampuni ya Mbolea Tanzania

KIWANDA CHA KUZALISHA MBOLESA KUJENGWA MKOANI SONGWE

Imewekwa: 19 May, 2025
KIWANDA CHA KUZALISHA MBOLESA KUJENGWA MKOANI SONGWE

Mkurugenzi wa Uendeshaji Biashara, Kampuni ya Mbolea Tanzania Bw. Lameck Borega amekutana na Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe. Daniel Chongolo ili kueleza malengo ya Serikali ya kujenga kiwanda cha uzalishaji wa mbolea zinazotokana na madini ya phosphate mfano mbolea za DAP, TSP na SSP.

Katika kikao hicho, kilichofanyika katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe Bw. Borega ameeleza kuwa utafiti uliofanyika umebaini Mkoa wa Songwe una akiba ya madini ya rock phosphate ambayo ni malighafi muhimu katika uzalishaji wa aina hizo za mbolea.

Kwa upande wake Mhe. Chongolo ameeleza kuwa Mkoa wa Songwe uko tayari kutoa ushirikiano wa kutosha ili kuhakikisha kuwa Serikali inafanikisha ujenzi wa kiwanda hicho kikubwa cha mbolea. Pia amesisitiza umuhimu wa mradi huo utakaoinua uchumi wa mkoa na kuongeza tija kwa wakulima kupitia upatikanaji wa mbolea bora na kwa gharama nafuu.

Kikao hicho kilichofanyika jana tarehe 17.05.2025, kimehudhuriwa pia na Katibu Tawala Mkoa wa Songwe Bi. Happiness Seneda