Mafunzo ya kamati ya kudhibiti UKIMWI na magonjwa yasio ambukiza.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mbolea Tanzania TFC, Ndg. Samwel Mshote amefungua mafunzo ya Kamati za TFC (Kamati ya Kudhibiti VVU, UKIMWI na magonjwa yasiyoambukiza) yenye lengo la kuiwezesha Kamati hiyo na wajumbe Menejimenti kutekeleza majukumu yao ipasavyo.
Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ofisi, Mkurugenzi Mkuu, Ndg. Samwel Mshote ameeleza kuwa mafunzo hayo ni fursa nzuri ya kujifunza juu ya masuala ya afya, kwani afya inamgusa kila mtumishi.
“Natambua sio watumishi wote walioshiriki katika mafunzo haya hivyo kwa mtakaoshiriki mafunzo haya tuwe mabalozi wazuri kwa wenzetu ambao hawajashiriki mafunzo haya. Tutakapokuwa na vikao vya kiidara tuwashirikishe watumishi wenzetu juu ya elimu tutakayoipata hapa,” ameeleza Ndg. Mshote
Ameendelea kueleza kuwa mafunzo hayo ni takwa la kisheria la Serikali na Sera za Nchi kwani watumishi wanapojitambua na kulinda afya zao ni mtaji. Na katika kazi mtaji wa kwanza ni rasilimali watu.
Wawezeshaji wa mafunzo hayo ni Mtaalam kutoka Ofisi Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na Mtaalam kutoka Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS)