Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Kilimo

Kampuni ya Mbolea Tanzania

KATIBU MKUU WIZARA YA KILIMO ATEMBELEA BANDA LA TFC

Imewekwa: 19 Jun, 2025
KATIBU MKUU WIZARA YA KILIMO ATEMBELEA BANDA LA TFC

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Nd. Gerald Mweli leo tarehe 19.06.2025 ametembelea na kuzungumza na watumishi wa Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika viwanja vya Chinangali, Jijini Dodoma.

Akiwa katika banda la Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) ametaka kufahamu juu ya elimu inayotolewa kwa wakulima kuhusu mbolea, sambamba kufahamu idadi ya wadau wanaotembelea katika banda kujifunza juu ya elimu ya mbolea.

Kampuni ya Mbolea Tanzania inashiriki Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yenye Kauli Mbiu; Himiza matumizi ya mifumo ya kidigiti ili kuongeza upatikanaji wa taarifa na kuchagiza uwajibikaji