MKURUGENZI TFC AMEWATAKA WATUMISHI KUENDELEZA UBUNIFU KATIKA MSIMU MPYA WA KILIMO
MKURUGENZI TFC AMEWATAKA WATUMISHI KUENDELEZA UBUNIFU KATIKA MSIMU MPYA WA KILIMO
Imewekwa: 25 Oct, 2024
![MKURUGENZI TFC AMEWATAKA WATUMISHI KUENDELEZA UBUNIFU KATIKA MSIMU MPYA WA KILIMO](https://www.fertilizer.co.tz/uploads/news/fb556ad363ff4b343672b564bc3b0660.jpeg)
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) Bw. Samuel Mshote amewataka wataalam wa kampuni hiyo kuendeleza ubunifu katika biashara ya uuzaji na usambazaji wa mbolea ili kuendana na ushindani katika soko la uuzaji wa mbolea.
Akizungumza katika kikao cha Menejimenti, kilichofanyika leo Bw. Mshote ameeleza kuwa kwa sasa TFC ina uwezo wa kufanya kazi na makampuni makubwa tofauti na hapo mwanzo hivyo ni wakati wa kuongeza ufanisi zaidi ili kuzidi kuleta imani kwa wadau na kusisitiza juu ya ushirikiano.
Aidha, amesisitiza juu ya usimamizi na utoaji wa elimu kwa wakulima na wadau ili wazifahamu mbolea zinazouzwa na kusambazwa na TFC hali itakayosaidia kuwajengea uelewa katika matumizi sahihi ya mbolea hizo.