Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Kilimo

Kampuni ya Mbolea Tanzania

TFC YASHIRIKI KONGAMANO LA KIMATAIFA LA UCHUMI NCHINI URUSI

Imewekwa: 19 Jun, 2025
TFC YASHIRIKI KONGAMANO LA KIMATAIFA LA UCHUMI NCHINI URUSI

Mkurugenzi wa Uendeshaji Biashara, Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) Bw. Lameck Borega ameshiriki katika Kongamano la Kimataifa la Uchumi la St. Petersburg International Economic Forum linalofanyika nchini URUSI.

Ameshiriki kongamano hilo leo tarehe 19.06.2025, kongamano lililoongozwa na Mhe Doto Biteko (Mb) Naibu Waziri Mkuu wa Tanzania na Waziri wa Nishati ambapo Mkurugenzi wa Biashara amekutana na kufanya vikao na wazalishaji wakubwa wa Mbolea ambao ni PhosAgro na UralChem kwa lengo la kuhakikisha kuwa Serikali inapata mbolea ya uhakika, kwa wakati na kwa bei himilivu.

Kampuni ya PhosAgro na UralChem ni maarufu katika uzalishaji wa mbolea duniani.