TFC YASHIRIKI MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI

Viongozi na Wageni mbalimbali wakitembelea katika banda la Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) ili kujifunza elimu ya afya ya udongo, aina za mbolea za kutumia kutokana na afya ya udongo, matumizi sahihi ya mbolea na faida za kutumia mbolea ili kustawisha mazao, katika maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa Umma 2025.
Maadhimisho haya yanafanyika katika viwanja vya Chinangali, Jijini Dodoma, yamefunguliwa rasmi leo tarehe 17.06.2025 na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (Mb).
Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yameanza tarehe 16.06.2025 na yanatarajiwa kuhitimishwa 23.06.2025. Kauli Mbiu: "Himiza Matumizi Sahihi ya Mifumo ya Kidijiti ili Kuongeza Upatikanaji wa Taarifa na Kuchagiza Uwajibikaji".