Accessibility Settings

Text Size

Color Contrast

Language

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Kilimo

Kampuni ya Mbolea Tanzania

/ News

Bodi ya TFC Yapongeza Kulinda Mtaji Wakati wa Kuendesha Biashara ya Mbolea

Imewekwa: 13 December, 2025
Bodi ya TFC Yapongeza Kulinda Mtaji Wakati wa Kuendesha Biashara ya Mbolea

Katika kikao cha 8 cha Bodi ya Wakurugenzi, Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC), wameitaka Menejimenti kuendesha biashara ya uuzaji na usambazaji wa mbolea huku wakilinda na kukuza mtaji, ili biashara iwe endelevu.

Akizungumza katika kikao hicho kilichofanyika taehe 29, Novemba 2025 katika ukumbi wa ofisi, jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Dkt. Florens Turuka ameeleza kuwa mtaji uliotolewa na Serikali kwa lengo la kuwahudumia wakulima mbolea za ruzuku ulindwe na kuongezeka.

Aidha, Wakurugenzi wa Bodi wamesisitiza juu ya utendaji bora wa majukumu kwa watumishi, ili kufikia malengo yanayokusudiwa, na kuitaka Menejimenti kuainisha viashiria vya hatari katika biashara ya uuzaji na usambazaji wa mbolea nchini.