Ziara ya Wajumbe wa Bodi ya TFC Kuhakikisha Upatikanaji na Uwiano wa Bei za Mbolea
Imewekwa: 13 December, 2025
Ziara ya Wajumbe wa Bodi, Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) yatembelea vituo vya mauzo na maghala, imeendelea katika ghala la Makambako, Mkoa wa Njombe ambapo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Dkt. Florens Turuka (wa kwanza kutoka kushoto) amesisitiza juu ya uuzaji wa mbolea kipindi chote cha msimu wa kilimo.
Akizungumza mara baadaya kukagua ghala hilo, Novemba 2025, Dkt. Turuka ameeleza kuwa upatikanaji wa mbolea wakati wote kutamuwezesha mkulima kunufaika na mbolea ya ruzuku wakati wote anapohitaji.
Aidha, amesisitiza kuhusu kubandika bei za mbolea za ruzuku katika vituo vya mauzo, jambo linaloleta uwazi na kumsaidia mkulima kufahamu bei ya kila mbolea pale anapofika kununua mbolea.

