SIKU YA MBOLEA DUNIANI
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo (anayeshughulikia maendeleo ya mazao) Dkt. Hussein Mohamed Omar ambaye pia ndiye mgeni rasmi katika kilele cha maonesho ya Siku ya Mbolea Duniani ameitaka Kampuni ya Mbolea Tanzania kuanza kufungasha mbolea ya ruzuku katika uzito wa kilo 5, 10, 20 na 25 ili wakulima wote waweze kunufaika na mbolea ya ruzuku kulingana na uhitaji wao.
Amesema hayo alipotembelea banda la Kamouninya Mbolea Tanzania kwenye kilele cha maonesho ya Siku ya Mbolea Duniani kwa kueleza kuwa wapo wakulima wadogowadogo ambao kilimo chao hakiitaji mbolea za kilo 50 hivyo ni vema TFC kuwafikiria kwa kuwa na vifungashio vya ujazo tofautofauti.
Akifafanua juu ya suala hilo, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) ameeleza kuwa kwa mwaka huu wa fedha 2024/2025 TFC inajenga kiwanda cha kuchanganya mbolea karibu na bandari ya Dar es salaam, hadi sasa tayari mchakato wa manunuzi unaendelea kiwanda hicho kitakapokamilika TFC itakuwa na uwezo wa kufungasha mbolea katika ujazo mbalimbali kulingana na mahitaji ya wakulima.