Accessibility Settings

Text Size

Color Contrast

Language

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Kilimo

Kampuni ya Mbolea Tanzania

/ News

Kampeni ya Mali Shambani Yaendelea Itilima na Bariadi, Simiyu

Imewekwa: 13 December, 2025
Kampeni ya Mali Shambani Yaendelea Itilima na Bariadi, Simiyu

Kampeni ya Mali Shambani imeendelea kwenye vijiji vya Nyamalapa, Banehmi, Budalabujiga, Gilya na Masewa katika wilaya za Itilima na Bariadi, mkoani Simiyu.

Hamasa kubwa kutoka kwa wakulima zaidi ya 500 wamejitokeza kusikiliza elimu kuhusu matumizi sahihi ya mbolea na namna ya kutambua mbegu feki.

Maafisa Ugani wa wilaya, pamoja na wataalamu kutoka Wizara ya Kilimo, Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), TOSCI, Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) na MMFL wameendelea kutoa mafunzo ya kina kwa wakulima na kujibu maswali.