Viongozi wa Taasisi chini ya Wizara ya Kilimo walioshiriki katika Mkutano Mkuu wa Nchi za Bara la Afrika.
Viongozi wa Taasisi chini ya Wizara ya Kilimo walioshiriki katika Mkutano Mkuu wa Nchi za Bara la Afrika.
Imewekwa: 09 May, 2024
Viongozi wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Kilimo TARI, TFRA, TFC na Agri Transformation wameshiriki katika Mkutano Mkuu wa Nchi za Bara la Afrika unaohusu Mbolea bora na Afya ya udongo.
Mkutano huu unaofikia kilele chake leo tarehe 9 Mei 2024 unaofanyika jijini Nairobi, Kenya wenye Kauli Mbiu “Listen to The Soil” umehusisha Wakuu wa Nchi, Mawaziri, Viongozi wa Jumuiya za Kikanda na Wakuu wa Taasisi.
Azimio la Nairobi ambalo limelenga kuboresha mkakati wa matumizi sahihi na kwa wakati ya Mbolea na kuimarisha Afya ya udongo linatarajiwa kusainiwa katika kilele cha mkutano huu ili kuwawezesha wakulima kuongeza tija ya uzalishaji mazao, kuongeza usalama wa chakula, kuimarisha kipato na kupunguza umaskini.