Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Kilimo

Kampuni ya Mbolea Tanzania

UKIDHIBITI VIASHIRIA VYA HATARI, HUTAPATA HOJA ZA UKAGUZI

Imewekwa: 08 Jul, 2025
UKIDHIBITI VIASHIRIA VYA HATARI, HUTAPATA HOJA ZA UKAGUZI

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC), Ndg. Samuel Mshote ameeleza kuwa pamoja na kuwa na mpango wa Viashiria vya Vihatarishi wa Kampuni ni vema mpango huo ukuwa unafanyiwa tathmini kila robo mwaka ili kubaini jambo kabla halijatokea.

Akizungumza na washiriki wa mafunzo ya  Viashiria vya Vihatarishi, yaliyotolewa na wataalam kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe, yaliyofanyika kwa siku 3 katika ukumbi wa ofisi za TFC, Ndg. Mshote ameeleza kuwa mafunzo hayo ni muhimu sana katika kujenga ustawi wa Taasisi.

“Ukithibiti viashiria vya hatari, kazi zako zitakuwa salama. Hutakwama wala hutapa hoja za ukaguzi,” ameeleza Ndg. Mshote

Aidha, amewasihi washiriki kuzingatia mafunzo waliyojifunza ili kuja kuitumia elimu hiyo katika utendaji kazi.