Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Kilimo

Kampuni ya Mbolea Tanzania

Mkutano wa Nchi za Bara la Africa unaohusu Mbolea na Afya ya Udongo Nchini Kenya

Imewekwa: 09 May, 2024
Mkutano wa Nchi za Bara la Africa unaohusu Mbolea na Afya ya Udongo Nchini Kenya

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) Bw. Samuel A Mshote akishiriki katika Mkutano Mkuu wa Afrika kuhusu Mbolea na Afya ya udongo. 

Lengo la mkutano huu ni kujadili na kupitisha Mkakati wa miaka 10 wa mapendekezo ya kisera na uwekezaji utakaowezesha uimarishwaji afya ya udongo na matumizi bora ya mbolea katika kuongeza tija katika kilimo katika nchi zote za Afrika (Nairobi Declaration). 

Mkutano huu umehusisha Wakuu wa Nchi , Mawaziri na Viongozi mbalimbali, unafanyika kwa siku tatu kuanzia tarehe 7-9 Mei, 2024, jijini Nairobi Kenya.