Ushiriki wa TFC kama Mdau katika Mkutano wa Wabunge Wanawake FP-ICGRL (WPC) umetambuliwa kwa kuimarisha kilimo, ukuaji wa uchumi na usalama wa chakula katika Ukanda wa Maziwa Makuu
Imewekwa: 15 May, 2026
Mkurugenzi Mkuu wa TFC, Bw. Samuel Mshote, amesisitiza umuhimu wa mbolea bora katika kuongeza tija ya uzalishaji wa kilimo na kuboresha maisha ya wananchi. Ameeleza kuwa TFC itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo katika kuhamasisha kilimo endelevu na chenye kuhimili athari za mabadiliko ya tabianchi.

